Siri ya Mbuzi wa Kinondoni Makaburini...Je ni Kweli ni wa Kichawi ? - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Jul 2015

Siri ya Mbuzi wa Kinondoni Makaburini...Je ni Kweli ni wa Kichawi ?

Kumekuwa na "story" nyingi juu ya mbuzi wanaolala maeneo ya Kinondoni makaburini,na wakati wa mchana kuzunguka huku na kule kuanzia Kinondoni muslim,studio,mpaka maeneo ya Biafra na Morrocco(?),hawa ni mbuzi wasio na mchungaji wala "mmiliki",huzunguka hapa na pale ktk kujitafutia malisho ktk majalala na maeneo ya makazi ya watu.

Wenyeji wengi wa Kinondoni wanasema mbuzi hao walianza kuonekana mmoja mmoja lkn sasa wamekuwa wengi na kuzunguka wakiwa ktk kundi.Hawachinjiki wala kukamatika,wengine huwahusisha na "masalia" ya mbuzi wa "kafara" ambapo watu wengi wanaoamini juu ya kafara huja nyakati za usiku ktk maeneo ya makaburi na kutoa kafara au kuwaacha kama njia ya kutawanya "mikosi" na "mabalaa".

Zipo habari za kikundi cha mateja kujikusanya na kuwakamata hao mbuzi na kuwauza kwa wapika supu,kitu kilichopelekea mateja wengi kupukutika kwa kifo na magonjwa ya hatari,na wale wanunuzi kupata mauzauza ya ajabu..kiasi mpaka sasa,licha ya njaa za mateja,lkn huwezi kukuta teja anawakamata na kuwauza.

Mbuzi Hawa Wanaitwa gusa unate...Je kwa wajuzi na wajanja wa Kinondoni,kuna ukweli gani juu ya mbuzi hawa??ni nani kweli mmliki wa hii mifugo?