Diamond: Hakuna Msanii Ambaye Nimewahi Kumlipa Wala yeye Kunilipa Kufanya Collabo - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Jul 2015

Diamond: Hakuna Msanii Ambaye Nimewahi Kumlipa Wala yeye Kunilipa Kufanya Collabo

Diamond Platnumz amesema kuwa ameshafanya collabo na wasanii A-list karibu wote wanaofanya vizuri Afrika, lakini hakuna hata mmoja ambaye amewahi kumlipa wala wao kumlipa kwaajili ya collabo hizo.

“Nimefanya collabo na wasanii tofauti tofauti, karibuni A-list wote ya wanaofanya vizuri Afrika nimeshafanya nao.” Alisema kupitia XXL ya Clouds Fm.

Ameongeza kuwa mwanzoni haikuwa rahisi kufanya nao kutokana na kwamba wengi walikuwa hawamfahamu tofauti na ilivyo sasa.

“Kiukweli sijawahi kufanya malipo ya mtu yoyote kufanya naye nyimbo. Mwanzoni wakati naanza kufanya ilikuwa kidogo tabu kwasababu mtu alikuwa hajafahamu anafanya nyimbo na nani, lakini sasa hivi wanafahamu kwamba…nikifanya nyimbo na Diamond, East Afrika mimi kwangu inakuwa kiurahisi nyimbo yangu, na upande wangu mimi inakuwa ni rahisi kwa West, kwahiyo tukichanganya inakuwa rahisi zaidi.

"Kwahiyo hakuna mtu ambaye nimeshawahi kumlipa wala yeye mimi kunilipa hii ni uongo sijawahi kufanya hivyo.”