Diamond Platnumz Aamua Kuungana na Wema Sepetu Kumpigia Kampeni Mgombea wa CCM John Magufuli - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Aug 2015

Diamond Platnumz Aamua Kuungana na Wema Sepetu Kumpigia Kampeni Mgombea wa CCM John Magufuli

Kutokana na demokrasia kila mtu ana haki ya kumchagua kiongozi ambaye anadhani kuwa anafaa bila shinikizo la mtu, hii imetokea pia kwa baadhi wasanii ambao wamegawana katika makundi ambapo kuna baadhi wapo team Lowassa na wengine team Magufuli.

Hadi sasa kuna baadhi ya mastaa wa Tanzania, wameweka wazi watu wanaowakubali kati ya wagombea wawili, miongoni mwao ni Wema Sepetu aliyeweka wazi kumsupport Magufuli, muigizaji Jacqueline Wolper na Aunty Ezekiel wanamsupport Edward Lowassa na sasa ni Diamond ameweka wazi kuwa yupo team Magufuli.

Kupitia mtandao wa kijamii Diamond ameandika “Iwe Msanii, Mtangazaji, ama Mwanamichezo, ila Kila Mtanzania anahaki ya Kuchagua kiongozi anaeamini ni Bora, Mchapa kazi, Mwenye Afya na Msimamo ili kutuendelezea Nchi yetu… Kwa Uchunguzi na tathmini niliyoifanya tangu hizi mambo za Kampeni zianze nimegundua na kuamini kuwa huyu ndio Jembe,”.

Akamalizia “Nitakuandikia na kukupostia ushahidi kukuthibitishia kwanini nimeona John Magufuli Pombe ndie anaefaa… unapohisi na wewe una fact za kumtetea umtakaye karibu uniambie hapo halaf na mi nikumwagie zangu, ila usijisumbue Matusi coz hayatokusaidia wala kunisaidia kunibadilisha akili yangu kwa sababu sanasana ntakuona Huna akili Maana nishayazoea, nipe fact zako nami nikupe zangu ili pamoja Tujenge nchi….. #HapaKaziTu #Ccm,”.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI