Jamani Zari Hajawahi Kuolewa – Diamond Platnumz - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Aug 2015

Jamani Zari Hajawahi Kuolewa – Diamond Platnumz

Diamond Platnumz amesema Zari hajawahi kuolewa na kwamba hadi sasa hajapokea barua yoyote kutoka mahakamani ikimtaka kuchukua vipimo vya DNA vya mtoto wake, Tiffah.

Kwa mujibu wa Diamond, barua iliyowekwa kwenye akaunti ya King Lawrenc ni moja ya njia ya swahiba hiyo wa ex wa Zari, Ivan ya kujipatia umaarufu.

“Sijapokea barua yoyote,” Diamond ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM leo.

“Unajua lazima tujue kila mtu anatumia mitandao kwa njia zake. Wengine wanatumia kutafutia umaarufu kama hivyo which is not bad but kupata umaarufu ni kazi sio, mtu anatafuta njia yoyote kutafuta umaarufu na watu wakamsikiliza na kupata pongezi kwa sababu amekaa amebuni kitu mpaka watu wakamsikiliza,” amesema Diamond.

“Zari hajawahi kuolewa kwanza, ni story tu hizo, lakini hajawahi kuolewa, ukimuuliza mwenyewe anasema hajawahi kuolewa kabisa,” amesisitiza staa huyo.

“Unapokuwa na mahusiano na mtu huwezi kufuatilia vitu vyake vya nyuma. Tumeanza maisha yangu mimi na yeye sidhani kama umeshaona post yangu yoyote ya kumzungumzia vibaya ndio maana nikiona vitu ambavyo navisikia naona ni uongo, mimi sifuatilii maisha ya mtu.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI