Utani Huu: Mpambe wa Ex wa Zari Anataka DNA ya mtoto wa Diamond, Anadai yeye ni Baba, Juzi Alidai Ivan Ndio Baba! - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Aug 2015

Utani Huu: Mpambe wa Ex wa Zari Anataka DNA ya mtoto wa Diamond, Anadai yeye ni Baba, Juzi Alidai Ivan Ndio Baba!

Guys kuna mambo mengi sana feki yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii. Tena zaidi ni kuwa mengi yanakuja na picha zinazoashiria ukweli lakini katika maisha ya chuki na visasi, kila kitu kinawezekana.

Bahati mbaya tunaishi kwenye dunia ambayo watu huamini haraka mambo hasi ambayo kwa kawaida husambaa haraka zaidi kuliko yale chanya. Na kwakuwa mitandao ya kijamii katika miaka ya hivi karibuni imekuwa chanzo kikubwa cha habari, blogs zimekuwa zikiwahiana kuandika habari na wakati mwingine bila kuzitafakari na kuzichuja vyema kupata uhalali wake.

Habari ya mpambe wa ex wa Zari, King Lawrenc, imetawala magazeti na blogs nyingi za Afrika Mashariki leo.


Lawrenc alipost kwenye akaunti ya Instagram kile kinachoonekana kuwa ni barua ya kutaka kufanyika vipimo vya DNA ili kujulikana ukweli wa nani ni baba wa Latiffah, ambaye ni binti wa Diamond Platnumz.

Lawrenc ametumia kampuni maarufu ya wanasheria ya nchini Uganda iitwayo WEB Advocates & Solicitors kumtaka Zari achukue vipimo vya DNA vya Tiffah katika nchi tatu tofauti ili kubaini nani ni baba wa mtoto huyu!

The funny part of this story is; Katika barua hii Lawrenc anadai kuwa yeye ndio baba wa mtoto huyu wakati katika post mbili zilizopita amekuwa akipost vijembe kuwa Tiffah ni mtoto wa Ivan, ex wa Zari. Ivan na Lawrenc ni marafiki!

Katika post ya kwanza, King aliweka picha ya Ivan na mtoto mchanga na kuandika, “No DNA Needed. The best revenge has shown itself after 9months.” Katika picha nyingine ambayo anaonekana akifurahia Cigar na Ivan, jamaa aliandika, “Chilling with @princess_tiffah’s father.”

Habari ya kuwa Ivan ndio baba wa Tiffah imebadilika, na sasa yeye ndiye anayelalamika kuwa ‘amenyimwa haki ya kumuona mtoto’ ambaye anaamini kuwa ni wake!

King Lawrenc ni mtu anayejulikana kwa njaa ya umaarufu na yupo radhi kufanya lolote ili aupate hata ikiwa ni kusema kuwa amewahi kulala na mke wa zamani wa rafiki yake, Ivan! Kinachowashangaza zaidi watu wengi ni kuwa Ivan anaruhusu yote haya.

Ivan yuko sawa kumuona mpambe wake akitangaza hadharani kuwa naye amewahi kutembea na Zari! Urafiki gani huu? Uhusiano wa Ivan na Lawrenc unatia mashaka sana!

Inavyoonekana Ivan na Lawrenc wamedhamiria kuhakikisha kuwa Zari na Diamond hawaipati ile furaha ya kupata mtoto. Hata hivyo hakuna chochote kati ya haya yanayoendelea kinachoonesha kuwaumiza Zari na Diamond.


Hatujui kinachoendelea ‘behind closed doors’ lakini picha za kwenye Instagram zinaonesha kuwa familia ipo katika kilele cha furaha. Diamond anaonekana kuwa baba anayejivunia kwa binti yake Tiffah.

Mungu akiepushe kichanga hiki na drama za watu wasiokuwa na mshipa wa aibu! Ama kweli umaarufu ni mzigo wa miiba!
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI