Makapi Aliyosema Mh. Kinana Haya Hapa - MULO ENTERTAINER

Latest

5 Aug 2015

Makapi Aliyosema Mh. Kinana Haya Hapa

“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi? - Kinana 04/08/2015

Wadau kutokana na kauli ya Mh Kinana aliyoitoa wakati akihutubia wanaCCM waliofika Lumumba kumsindikiza Mh Dr John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya uraisi wa JMT, alimaanisha kwamba kila aliyetia nia ya uongozi CCM na hakupata fursa hiyo ni makapi. Nijuavyo makapi ni mabaki yeyote baada ya mchujo/mchakato.

Katika mchakato ule kulikuwa na watia nia 42 na baadae 38 walifanikiwa kurudisha fomu. Katika mchujo ule ni Magufuli pekee aliibuka kidedea baada ya michujo kadhaa. Kwa mantiki hiyo aliyepita kwenye chujio ni Magufuli na wengine waliobaki ndiyo MAKAPI. Kama nilivyomwelewa Mh Kinana ina maana hao MAKAPI hata wakishindana na mgombea wao sehemu yeyote ile hawatashinda.
Kwa mujibu wa Mh Kinana alimaanisha hivi:

A. Mgombea
1. John Pombe Magufuli

B: MAKAPI ( Waliobaki baada ya mchujo)Kwa kuwa hakuna mgombea yeyote aliyefukuzwa CCM baada ya mchakato wa kumtafuta mgombea uraisi kwa Chama Cha Mapinduzi kukamilika, neno MAKAPI linabaki kuwahusu wale wote waliochujwa kwenye mchakato na yeyote (makapi) akishindana na mgombea popote pale watashindwa.
Ifuatayo ndiyo listi ya MAKAPI kulingana na kauli ya Mh Kinana:

Bilal
Lowasa
Pinda
Mwakyembe
Sitta
Nyalandu
Mwigulu
Makamba
Kigwangwala
Chikawe
Ali Karume
Mwandosya
Amina Salum Ally
Asha Rose
Membe
Wassira
Makongoro
Ngeleja
Mpina
Sumaye
Muhongo
Sanoko
Mahiga
Jaji Ramadhani
Dr Mwele
Murenda
Boniface Ndembo
Bw Bilohe (Mkulima)
Peter Nyalali
Helen Elinewinga
Anthony Chalamila
Dk Muzamil Kalokola nk.