Nuh Mziwanda: Wengi Walimshauri Shilole Aniache - MULO ENTERTAINER

Latest

7 Aug 2015

Nuh Mziwanda: Wengi Walimshauri Shilole Aniache

Msanii wa Bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Ganda la Ndizi' Nuh Mziwanda akiwa na mchumba wake Shilole amefunguka na kusema watu wengi walimshauri mpenzi wake huyo amuache.

Nuh amesema watu walimpatia ushauri huo Shilole, baada ya hivi karibuni kusambazwa sauti yake katika mitandao ya jamii akisikika kumtaka kimapenzi msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu, mazungumzo yao yalikuwa yamerekodiwa kwa njia ya simu na kusambazwa na mtu asiyejulikana.

Nuh Mziwanda amesema baada ya sauti hiyo kusambazwa watu wengi walikuwa wakimpigia simu Shilole na kumshauri aachane naye lakini anamshukuru Mungu, Shilole hajaweza kuwasikiliza na wanaendelea poa na maisha yao kama wapenzi na kudai Mungu ana kusudio lake kufanya waendelee kuwa pamoja.

"Wengi mlishauri aachane na mimi, ila Mungu ana kusudio lake kufanya tuendelee kuwa pamoja na nampenda sana Shishi wangu na sifikirii kumuacha," alisema Nuh Mziwanda.

Baada ya kauli hiyo ya Nuh Mziwanda mashabiki wake katika mitandao ya jamii walimbadilikia na kusema kuwa anapenda sana mteremko na kutafutiwa ndiyo maana anahangaika na watu ambao wamemzidi umri, huku wengine wakionyesha kutopenda mambo yake ya ndani anavyoanika katika mitandao ya kijamii hususani kuhusu mapenzi yake na mchumba wake.