Steve Nyerere Awaumbua Mastaa Wasio ipigia Kampeni CCM - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Aug 2015

Steve Nyerere Awaumbua Mastaa Wasio ipigia Kampeni CCM

Steve Nyerere na Wema Sepetu
STAA wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewachana wasanii kwa kuwaita wanafiki kutokana na kuukacha uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Uwanja wa Jangwani wiki iliyopita.

Akizungumza na mwandishi wetu juzikati, Steve alisema ameshangazwa kuona baadhi ya wasanii kuikacha CCM na kuupigia debe Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vinne vya Chadema, Cuf, NCCR na NLD wakati Serikali ya CCM imewafanyia mambo makubwa.

“Hawa wasanii ni wanafiki na ndiyo maana wakati mwingine unatakiwa kuwaambia ukweli tu. Serikali ya CCM imetufanyia mambo mengi kwenye sanaa na kwa kutambua hilo ndiyo maana juzi tulimuaga kwa kishindo rais Jakaya Kikwete lakini baadhi ya wasanii tuliokuwa nao katika hafla hiyo nao wanaiponda CCM na kushabikia Ukawa,” alisema Steve bila kuwataja majina.

Miongoni mwa wasanii ambao wamejipambanua moja kwa moja kuwa ni Ukawa ni pamoja na Aunt Ezekiel, Chuchu Hans, Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine kibao.