TCRA Watoa ADHABU Kwa Kituo cha Televisheni cha ITV - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Aug 2015

TCRA Watoa ADHABU Kwa Kituo cha Televisheni cha ITV

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa  adhabu ya onyo  kali  na  kukitaka  kituo cha  ITV kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi (pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo  Muyangi  alisema kamati hiyo imebaini kituo cha  ITV kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini kwa kurusha taarifa ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini.

Alidai katika kipindi cha Habari zilizotufikia muda huu kilichorushwa siku ya Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi , ITV  Walitangaza  “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais."

Alisema katika kipindi hicho Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya kubaini yanauvunjifu wa amani huku Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akidai ndo amesema hivyo,Wakati taarifa hiyo ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo halikuwa limetoa taarifa hizo..

Bi Muyangi  alisema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya kwanza juu kuzuiliwa  huko kwa maandamano, ndipo siku hiyo hiyo  tena katika kipindi hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu asubuhi kilirushwa taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu maandamo ya Chadema kutoka Makao makuu wa Chama cha Wananchi CUF Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Muyangi alidai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya Kamanda Kova juu ya kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza ambayo haikuweka uthibitisho wa Kamanda Kova.

Alisema baada ya Mamlaka hiyo kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na Mkurugenzi wa ITV Bi Mhavile na mkurugenzi wa Redio one Deogratus Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa ili kutaka  ufafanuzi ambapo wote kwa pamoja walikiri kosa hilo huku wakisema Mtangazaji huyu alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ilikuwa inakataza maandamano hayo ambapo alishindwa  kuithibitisha kama taarifa hiyo  ni ya kweli au la.

Aidha, Bi Muyangi alisema baada ya Kamati hiyo kusikiliza pande zote,ndipo wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha taarifa zinazoleta mchanganyiko katika jamii,