Basata Yadai Adhabu Ya Shilole Ipo Pale Pale,Ushahidi Unakusanywa Kumtwanga Nyundo Kali Zaidi - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Sept 2015

Basata Yadai Adhabu Ya Shilole Ipo Pale Pale,Ushahidi Unakusanywa Kumtwanga Nyundo Kali Zaidi

Shilole
Shilole anaweza akawa anafurahia bata za Marekani baada ya kutumbuiza kwenye show nchini humo, lakini bado BASATA haijamalizana naye.
Katibu Mtendaji wa baraza la sanaa la taifa, BASATA, Geofrey Mngereza ameiambia Radio 5 ya Arusha kuwa adhabu aliyopewa Shilole ya kufungiwa kutojihusisha kwenye masuala ya sanaa kwa mwaka mmoja haijafutwa. 
Mngereza alidai kuwa adhabu iliyotolewa kwa Shilole imetokana na sheria na kanuni zilizotokana na bunge na kwamba kwa sasa wanakusanya ushahidi ili kuchukua hatua. 
“Litachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosema,” alisema Mngereza. 
“Kwahiyo itapitia process ile ile ambayo imetumika hapo awali kuweza kutoa adhabu. Kwahiyo ni kitu ambacho kinafanyiwa kazi.”