Magufuli Kasema Chanzo cha Mgao wa Umeme Nchini ni Wagombea Urais wa Upinzani Ambao Wamepiga Dili na Kampuni za Umeme - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Oct 2015

Magufuli Kasema Chanzo cha Mgao wa Umeme Nchini ni Wagombea Urais wa Upinzani Ambao Wamepiga Dili na Kampuni za Umeme

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kuwa tatizo la umeme linaloendelea nchini limesababishwa na baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani.

Mgombea huyo wa CCM aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana mkoani Lindi na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho, ambapo alisema kuwa baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ndio chanzo cha tatizo la umeme nchini kwa kuwa ‘walipiga deal’ kupitia makampuni ya ufuaji umeme.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magufuli, alisema amepata taarifa kwamba kuna njama zinaandaliwa kwa lengo la kumuangusha mgombea ubunge Jimbo la Mtama kwa tiketi ya chama hicho, Nape Nnauye.

Dk. Magufuli aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mtama mkoani Lindi.

Alisema Nape anaandaliwa njama ili asipite katika kinyang’anyiro cha ubunge jimboni humo kwa sababu aliwataka baadhi ya wana-CCM wajivue gamba wakati chama hicho kikiwa katika mchakato wa kufanya mabadiliko.

Hata hivyo, Dk. Magufuli alisema Nape ni kiongozi mzuri ambaye endapo yeye (Dk. Magufuli), angekuwa na uwezo wa kumhamisha,  angemhamishia kwenda kugombea katika jimbo lake la Chato.