Rayuu Afunguka Kuhusu Wanaume Wanne Waliomfanyia Mbaya Kisha Kumtosa Bila Kumuoa - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Oct 2015

Rayuu Afunguka Kuhusu Wanaume Wanne Waliomfanyia Mbaya Kisha Kumtosa Bila Kumuoa

NYOTA wa filamu Alice Bagenzi ‘Rayuu’ amesema anajihisi kama mwanamke mwenye mkosi baada ya wanaume wanne alioshiriki nao mapenzi kuonesha nia ya kumuoa, lakini ghafla waliingia mitini na kupeperusha ndoto yake ya kuwa mke wa mtu.

Akipiga stori na gazeti hili, muigizaji huyo alisema umri wake unamruhusu kuolewa na anafanya kila njia ikiwa ni pamoja na kutii maelekezo yote ya mwanaume ili kumvutia aingie naye katika ndoa, lakini kinachomshangaza hubadilika ghafla na kumpotezea kabisa.
“Siyo siri naumia sana, huenda nimerogwa nisiolewe, mwanaume anajitambulisha hadi kwa wazazi na kuanza mchakato wa ndoa lakini baadaye anaingia mitini,” alisema Rayuu