Waandaji wa Tuzo za The Future Awards Africa ‘TFAA’ wametangaza mabalozi wa maadhimisho ya 10 ya Tuzo hizo, mabalozi hao ni pamoja na watu waliowahi kushinda Tuzo hizo kwenye upande wa biashara, maendeleo, utawala bora, burudani na ubunifu kwenye viwanda.
TFFA imechagua mabalozi 10 ikiwemo mwanamuziki Diamond Platnumz (Tanzania) , Mjasilia mali, Patrick ngowi (Tanzania), Muandaaji wa muziki Michel ‘Don Jazzy’ Ajere (Nigeria), muimbaji wa kimataifa Bukola ‘Asa’ Elemide (Nigeria), Mjasilia mali wa urembo ara Fela Durotoye(Nigeria), mwanzilishi wa LEAP AfricaNdidi Nwuneli (Nigeria), Mwekezaji kwenye kilimo Nnaemeka Ikeguonu (Nigeria), Mwanaharakati Sangu Delle (Ghana), Mwanamabadiliko Fogblanbenchi Lily Harity(Cameroon), Mbuge Oramait Alengoil (Uganda).
Mwanachama wa kamati kuu ya Tuzo hizo, Sean Obedih amesema wamewateuwa mabalozi hao kumi kwasababu Kazi zao na maisha yao yameshawashawishi Mamilion ya watu wengine kufanya kazi kwa ajili ya amaendeleo ya jamii zao.
“These 10 African icons have been selected from across East, West and Southern Africa because they represent the essence of TFAA. They speak to the best that Africa has, but more importantly their lives work have inspired millions to take charge of their destinies and to get involved in rebuilding their communities and their countries.There are no better ambassadors than these to drive our #AfricaNeedsYou message as we celebrate 10 years of the awards and prepare for 10 more years of impact.” Alisema Sean Obedih
Tazama Picha za Mabalozi wote wa Tuzo hizo