Msanii wa muziki wa kizazi kipya Aslay Isihaka amefunguka kuwa anapesa inayotosha yeye kubadili mboga.
Aslay ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na eatv.tv ambapo amesema kuwa pesa anayo lakini sio ya kutisha sana inatosha kukidhi mahitaji yake na familia yake.
“Pesa ninayo ya kubadilishia mboga nisiseme sina kabisa ntakuwa nakufuru, inatosha kukidhi mahitaji yangu na familia yangu”.
Hivi karibuni msanii huyo alitajwa katika kundi la wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye pesa nchini zinazotokana na kazi zao.