CCM Yalaani Vijana 1500 Kujitangaza Mashoga Mkoani Iringa - MULO ENTERTAINER

Latest

4 Jan 2016

CCM Yalaani Vijana 1500 Kujitangaza Mashoga Mkoani Iringa

Chama  Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa kimewataka vijana waliopo wilayani  humo kuacha  kujihusisha na masuala ya ushoga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi,Jimson Mhagama alisema hatua ya vijana kuingia katika ushoga ni sawa na kulidhalilisha taifa.

Kauli ya Mhagama imekuja mara baada ya kuwepo kwa taarifa za vijana  na wanafunzi 1500  wa  elimu ya juu waliopo mkoani humo kujihusisha na vitendo vya ushoga, hali ambayo imeleta taswira mbaya.

Alisema ni vyema vijana hao wakaacha tabia hiyo na badala yake watafute pesa kwa njia halali na si kujiingiza kwenye maswala ambayo yanavunja heshima ya jamii na taifa kwa ujumla.

"Wanafunzi wa Elimu  ya  juu wanaojihusisha  na  ushoga  wanadhalilisha vyuo  vyao  na  familia zao, lakini CCM inapendekeza kuwa mwanafunzi atakayebainika kufanya mchezo huo afukuzwe chuo mara moja" Alisema Mhagama

Alisema umefika wakati kwa Bunge kutunga sheria kali na kuifanyia mabadiliko katiba ya mwaka 1977  kuweka kipengele kinachobana  mambo  ya  ushoga.

Aliongeza,mtu akibainika ni shoga apewe adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela