Mkurugenzi wa Jamii Forums na mwenzake wakutwa na kesi ya kujibu - MULO ENTERTAINER

Latest

23 Feb 2019

Mkurugenzi wa Jamii Forums na mwenzake wakutwa na kesi ya kujibu


Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo na mwanahisa mwenzake, Micke William wamekutwa na kesi ya kujibu. Wanatuhumiwa kuzuia uchunguzi wa Polisi kwa kutotoa taarifa za wanachama wa JamiiForums, kutokutumia kikoa cha .tz, na kuzuia upelelezi wa Polisi unaohusiana na CRDB.

Ikumbukwe kuwa, mnamo Juni 01, 2018 shauri jingine namba 457 kama hili (lilihusu Kampuni za Cusna Investment na Ocean Link kuandikwa JamiiForums (sawa na Olicom (T) Ltd) kudaiwa kukwepa kodi bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania] washtakiwa waliachiwa huru na Hakimu Godfrey Mwambapa baada ya kukutwa hawana kesi ya kujibu.

Leo, upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Elia Atanas huku upande wa Utetezi ukiwakilishwa na Wakili Nashon Mkungu.

Katika shauri hili Maxence Melo na Micke William wataanza kujitetea mnamo Machi 14 na Machi 19 na upande wa utetezi umesema utakuwa na mashahidi wasiopungua 5.

Washtakiwa walishtakiwa kwa kuzuia uchunguzi wa Polisi kwa kushindwa kutoa taarifa muhimu za Mwandishi (Mwanachama wa JamiiForums aliyejulikana kwa jina la Fahrer) aliyeandika kuhusu kampuni ya OilCom (T) Ltd ikidaiwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta katika bandari ya Dar es Salaam.

Polisi walikuwa wakihitaji mambo manne kuhusu Fahrer ambayo walidai yatawasaidia katika uchunguzi, walihitaji Barua pepe ya Mwanachama huyo, namba za simu, IP Address pamoja na mada nyingine zote alizowahi kuanzisha mwanachama huyo. Shauri hili lilifunguliwa mnamo Desemba 16, 2016 pamoja na mashauri mengine mawili, shauri namba 457 na 458.