Magufuli Hakupiga Marufuku Uvaaji wa Sketi Fupi..Unaonea ni Uzushi Msidanganyike - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Jan 2016

Magufuli Hakupiga Marufuku Uvaaji wa Sketi Fupi..Unaonea ni Uzushi Msidanganyike

Wizara ya mambo ya nje nchini Tanzania imekanusha taarifa kwamba Rais John Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa sketi fupi maarufu kama vimini.

Taarifa ya Wizara hiyo imesema: "Ni kweli kwamba Rais Magufuli na Serikali yake wanaunga mkono uvaaji wa nguo za staha, lakini taarifa kwamba Rais Magufuli amepiga marufuku uvaaji wa sketi hizo fupi si za kweli.”

Tangu Jumatatu wiki hii, mitandao ya kijamii ilirindima na taarifa kwamba Rais Magufuli ametangaza marufuku hiyo.

Wizara ya Mambo ya Nje imelishutumu gazeti moja la Kenya kwa kuanzisha uvumi huo, na kukiita kitendo hicho kuwa "si cha umakini”.

"Wakati serikali ikifurahishwa na taarifa nzuri za utaendaji kazi wa Rais Magufuli katika vyombo vya habari vya Kenya na ulimwenguni kote, Wizara ya Mambo ya Nje imekerwa na utoaji wa taarifa potofu na zisizo makini kama hii ihusuyo sketi fupi," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Wizara hiyo hata hivyo imesema inaamini habari hizo hazikuchapishwa gazetini makusudi.