Babutale 'Nilipomuona Chid Benzi Mwanzo Kwa Jinsi Alivyo Sasa Nilidhani Msanii Huyo Ameathirika na UKIMWI..Lakini... - MULO ENTERTAINER

Latest

24 Mar 2016

Babutale 'Nilipomuona Chid Benzi Mwanzo Kwa Jinsi Alivyo Sasa Nilidhani Msanii Huyo Ameathirika na UKIMWI..Lakini...

Meneja wa msanii Diamond Platnum na kundi la Tip top Connection, Hamisi Taletale alimaarufu kama Babutale amefunguka na kusema kuwa alipomuona Chid Benzi mwanzo alidhani msanii huyo ameathirika na virusi vya UKIMWI

Akipiga stori kwenye kipindi cha Planet Bongo Babutale amesema kwa muonekano aliomuona nao Chid Benz hasa zaidi kwenye picha ambazo zilikuwa zikisambazwa kwenye mitando ya kijamii zilimtisha na kuhisi labda Chid Benzi anasumbuliwa na maradhi mengine kama ngoma.

"Kusema ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chid Benzi labda ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya ndiyo yamempelekea hali ile. Lakini sikuweza kuamini kesho yake ilibidi nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha afya na kufanya check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa" alisema Babu Tale

Katika hatua nyingine Babu tale amesema yeye ameamua kumsaidia Chid Benzi ili aweze kurudia katika hali yake ya kawaida na aendelee na maisha yake ya kawaida na si kusema ameamua kumsaidia kwa sababu ya kutafuta kiki au kutafuta maslahi kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai.