Diamond Aingia Studio Kumaliza Wimbo na Ne-Yo, Akutana na Hakeem wa Empire - MULO ENTERTAINER

Latest

8 Mar 2016

Diamond Aingia Studio Kumaliza Wimbo na Ne-Yo, Akutana na Hakeem wa Empire

Diamond hakwenda Las Vegas kutumbuiza tu bali pia ameitumia fursa hiyo kumalizia kiporo cha wimbo wake na Ne-Yo. Wawili hao walirekodi kwa mara ya kwanza wimbo wao mwaka jana jijini Nairobi lakini kuna vitu hawakumalizia.

Akiwa Las Vegas, staa huyo aliingia studio na Ne-Yo pamoja na producer, Jesse Corporal Wilson aliyeshiriki kutayarisha nyimbi nyingi za Ne-Yo.

Huenda pia akatumia fursa hiyo kufanya video ya wimbo huo.

Pia staa huyo alikutana na rapper na muigizaji wa Empire, Bryshere Y. Gray aka Yazz The Greatest anayejulikana kwenye tamthilia hiyo kwa jina la Hakeem.