Idris Afunguka, Aeleza Kinachoendelea Kuhusu Mahusiano yake na Wema Sepetu.. - MULO ENTERTAINER

Latest

19 Mar 2016

Idris Afunguka, Aeleza Kinachoendelea Kuhusu Mahusiano yake na Wema Sepetu..

Mshindi wa BBA, Idris Sultan amesema penzi lake mwigizaji Wema Sepetu lipo palepale na mwanadada huyo hana mtu mwingine wa Kikongo kama ilivyodhaniwa hivi karibuni.

Idriss amefunguka yote hayo katika mahojiano na kipindi cha 'Friday Night Live' kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa.

Akijibu swali la mtangazaji Sam Misago kuhusu mahusiano yake na Wema Sepetu kwa sasa kwamba inasemekana hawapo sawa Idris amesema
 ''Mimi na Wema Sepetu ni Mwaa bado tupo zizuri kabisa''
Alipoulizwa kama ni kweli anampenda Wema au anatafuta 'kiki' amasema ingekuwa anatafuta umaarufu wa namna hiyo basi angeamka asubuhi na kuandika asubuhi 'kiki day'

Kuhusu watoto ambao alisema walipotea kabla hawajazaliwa Idris amesema awamejifunza kitu kutotoa taarifa kabla ya ujauzito haujafika hata miezi 3 hadi 5.

Aidha kuhusu saa yake aliyoionyesha kwenye mitandao ya kijamii ambayo watu wanadhani ni feki Idriss ametamba kuwa saa yake ni 'original' na alipewa zawadi na mfalme mmoja barani Afrika.