Mbunge Sugu Awachana Wasanii Kufanya Show Ulaya....Adai Sio Kigezo Kwa Music Wetu Kukua - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Mar 2016

Mbunge Sugu Awachana Wasanii Kufanya Show Ulaya....Adai Sio Kigezo Kwa Music Wetu Kukua

Kwenye stori tatu ya Planet Bongo ya East Africa Radio, Sugu amesema huwezi kutumia kigezo cha wasanii kufanya show nje ya Afrika yaani Ulaya, America na kwengineko kama kigezo kuwa game imekua, kwa sababu show kama hizo walishazifanya miaka zaidi ya 20 iliopita.
“Huwezi kutoa credit kwa kusema wasanii wanaenda kupiga show Ulaya, Sugu, X-plastars, tumekwenda tour Europe miaka 20 iliyopita 18 au 17, kwa hiyo mimi sichukulii hiyo kama credit kama tour tulizokuwa tunapiga sisi, I apriciate hustle za kila mtu lakini sisi tulikuwa tunaenda kwenye mafestival ya dunia unapiga mbele ya mtu laki moja, ukirudi nyumbani hakuna suport kwa hiyo ili watu laki moja waliokuona kule wakupe thamani wanakuja kuangalia huko kwenu huko vipi unakuta watu wanakuzingua tu”, alisema Sugu.

Sugu kwa sasa ameachia wimbo wake unaoitwa freedom, baada ya kimya kirefu kilichosababishwa na yeye kuingia kwenye siasa, mpaka kufanikiwa kutwaa jimbo la Mbeya mjini.