Wimbo wa Nay wa Mitego Shika Adabu Yako Wavuka Mipaka...Mwanamuziki Amani wa Kenya Adai Anaupenda Sana..Asema Haya - MULO ENTERTAINER

Latest

11 Mar 2016

Wimbo wa Nay wa Mitego Shika Adabu Yako Wavuka Mipaka...Mwanamuziki Amani wa Kenya Adai Anaupenda Sana..Asema Haya

Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego inaweza ikawa imefungiwa na BASATA, lakini imefanikiwa kuwafikia watu wengi ndani na nje, shukrani kwa mitandao ya kijamii.


Na sasa muimbaji wa Kenya, Amani, amedai kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa wimbo huo.

“Naipenda sana,” alisema Amani kwenye kipindi cha Mseto cha Radio Citizen.

Amesema mstari uliomchekesha zaidi ni ule wa Ommy Dimpoz japo alisema staa huyo wa ‘Wanjera’ achukulie poa tu aliyoambiwa.

Amani anadai mstari mwingine anaoupenda ni ule Nay anasema wasichana wa mjini siku hizi hawavai nguo za ndani.

Mtazame mrembo huyo akiungolea wimbo huo.