Sababu za Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa Kwa Mwanamke - MULO ENTERTAINER

Latest

27 Jun 2016

Sababu za Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa Kwa Mwanamke

Ni kawaida kwa wanawake kuhisi   maumivu wakati wa kujamiiana. Katika matukio mengi   hali kama hizo, hutokana na mwanamke kutolainika sawasawa, hali hii inaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuongeza muda wa kumchezea mwanamke(foreplay) au kutumia vilainishi vya ziada. Hata hivyo, iwapo  maumivu hayakuweza kupungua, hizi hapa  ni baadhi ya sababu, ambazo  husababisha  maumivu  wakati wa tendo la ndoa:


Kukakamaa kwa misuli ya uke (Vaginismus): hali hii inasababishwa  na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha.

Matatizo ya shingo ya kizazi: Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu mara shingo ya kizazi inapogusana na uume.

Matatizo katika mfuko wa uzazi: Matatizo kama fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono.

Maambukizi ya uke: aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile  maambukizi ya fangasi inaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.

Kuumia uke: majeraha  kutokana na sababu kadhaa mfano kuchanika  wakati wa kujifungua au kuongeza njia katika msamba wakati wa kujifungua.

Endometriosis: Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za   mji wa mimba  kukua nje ya mfuko wa uzazi, na hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili.

Maambukizi kwenye funga nyonga(PID): Viungo kwenye nyonga vinaweza kupata maambukizi hivyo kusababisha   maumivu wakati wa ngono.

Matatizo ya ovari: Matatizo haya ni pamoja na uvimbe kwenye mfuko wa mayai (ovarian cyst)

Wanakuwa waliokoma siku(Menapause): Wakati wanapokuwa wamekoma siku zao maumbile yao yanasinyaa na  kuwa   kavu,  hivyo kuchochea maumivu wakati wa tendo la ndoa

Magonjwa ya zinaa:  magonjwa ya zinaa kama malengelenge (herpes), masundosundo n.k, yanaweza kusababisha maumivu wakati wa ngono.