Ukweli Kuhusu Tukio la Ngoma Kudaiwa Kumpiga Tambwe - MULO ENTERTAINER

Latest

26 Jun 2016

Ukweli Kuhusu Tukio la Ngoma Kudaiwa Kumpiga Tambwe


Kama ni mmoja kati ya watu waliosikia zile stori za washambuliaji wa Yanga wa kimataifa Donald Ngoma kutoka Zimbabwe na Amissi Tambwe kutoka Burundi kupigana ngumi, June 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Yanga Jerry Muro ameweka wazi ukweli wa tukio lenyewe.

“Kitendo hicho kinachosemwa sio cha kweli, wachezaji walikuwa kwenye mazoezi wakachezeana rafu kwa bahati mbaya, lakini Tambwe aliumia kidogo lakini habari kuwa waligombana sio kweli, Tambwe na Ngoma ifahamike kuwa hawagombanii namba, wote wapo kikosi cha kwanza”