Je Umesikia Kuwa Nahreel na Kundi la Weusi Haziivi? Nahreel Afunguka Ukweli Hapa - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Jul 2016

Je Umesikia Kuwa Nahreel na Kundi la Weusi Haziivi? Nahreel Afunguka Ukweli Hapa

Producer wa The Industry, Nahreel ameukata mzizi wa fitina kwa kukanusha kuwa na tofauti na Weusi.

Amedai kuwa kubadilisha mfumo wa kurekodi muziki kwenye studio zake hakujavunja uhusiano na wasanii hao.

“Kusema ukweli hakuna mtu aliyekimbia, sisi bado ni washkaji, we are family, na kiukweli nimebadilisha utaratibu wa studio lakini si kwamba nilivyobadilisha ile ikaleta utata fulani, hakuna,” Nahreel ameiambia Bongo5.
“Hii ni biashara na mimi sasa hivi nataka niisukume biashara yangu iende mbali zaidi, kwahiyo nilibadilisha utaratibu kidogo lakini hiyo sio sababu yake kusema leo Weusi wamenikimbia au Jux au nani. Wale ni washkaji hata sasa hivi tumetoka tu kuongea nao vizuri tu na kuna projects ziko pale, kuna nyimbo ya Davido na Joh Makini, kuna nyimbo Joh Makini anayo na Khuli Chana iko pale, kuna nyimbo ya G-Nako ameimba na Vanessa ipo, Jux ana nyimbo zake kwahiyo zitatoka soon,” amesisitiza.

Nahreel amedai kuwa hivi karibuni amekuwa busy na tour na mambo mengi ya kundi la Navy Kenzo na hivyo kupishana ratiba na wasanii hao lakini amesisitiza kuwa hakuna tofauti yoyote iliyopo.