Professor Jay: Kutokujua kimombo si dhambi - MULO ENTERTAINER

Latest

30 Jul 2016

Professor Jay: Kutokujua kimombo si dhambi

Msanii wa muziki wa Hip Hop na mbunge wa Mikumi, Professor Jay amesema kuwa kutokujua Kiingereza siyo dhambi.

Rapper huyo kwa sasa anakiki na wimbo wake mpya ‘Kazi Kazi’ aliomshirikisha msanii wa nyimbo za visingeli, Sholo Mwamba. Akiongea na kipindi cha Hatua Tatu cha Times FM, Professor Jay alisema, “Hii sijui kiingereza, Kiingereza ni Kushoboka tu. Viongozi wengi mbona tunaona wanakuja hapa Tanzania hawajui Kiingereza.”

Aidha kiongozi huyo ameongeza kuwa kwa wasanii mameneja ndio wanapaswa wajue lugha hiyo ili wawe kama wakalimani kwa wasanii wao.