Nimekuwa Mtumwa wa Wanawake - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Oct 2016

Nimekuwa Mtumwa wa Wanawake

Nimeficha ficha haya mambo ila najiona kabisa naangamia hivyo ni bora leo niombe ushauri maana hapa pana watu wazima, wanasaikolojia na viongozi wa dini.

Mkasa wangu ni wa hakika na bado nipo katika mateso hata sasa.

Wakati nipo balehe nilikutana na wasichana mbali mbali waliouteka moyo wangu na nikawaeleza hisia zangu, kwa bahati mbaya nilijibiwa karaha na kutoswa sababu ya maisha yangu ya dhiki.
Hali ilikwenda hivyo kwa muda mrefu mpaka moyo wangu ukajenga chuki na wanawake, niliwaona hawana usawa na sio wa kuwa nao karibu.

Katika utafutaji wangu wa maisha ghafla mambo yakabadilika na nikawa nina pesa na kuishi vizuri na nikaanza kujenga nyumba na pia nikawa na miradi pamoja na gari ya kutembelea.

Ni hapo ndipo wasichana wakaanza kuwa karibu na mimi na kunihitaji kimapenzi, na mimi nilishajenga chuki moyoni na nikapanga kuwakomoa, nikajikuta natembea na wanawake wengi tofauti kuanzia wanafunzi, walimu, wasichana tu wa mtaani, machangudoa na wapenzi wa watu.

Nikajikuta dhaifu mbele ya wanawake yaani siwezi kulala hata siku moja peke yangu bila mwanamke na pia mda mwingine nilifanya mapenzi na wasichana wawili tofauti kwa siku moja, haswa kama huyo wa pili aliyenitafuta ni mzuri sana.

Haya mambo sipangi bali najikuta tu inatokea na kila nikimaliza najuta na kusema ndio mara ya mwisho ila punde tu naingia katika vishawishi tena, nilioa mke safi kabisa ili niepuke hali hii ila tuliachana baada ya kunifumania mara kadhaa.

Sasa nina mke mwengine na safari hii nimeoa mke wa ndoto yangu mtoto mzuri sana shombe shombe kiasi kwamba marafiki wanasema kweli mwamba umepata kifaa.

Ila bado ninajikuta natembea na rafiki zake pia wasichana wa mtandaoni kama vile Jf, Badoo, Fb nk na pia nimekuwa maarufu madanguro mengi sana mpaka naona noma.

Mara kadhaa nasafirisha mademu wakali toka mikoa tofauti na kunifuata mimi, sihongi sana na wala sijatetereka ki uchumi na wala sijaathirika ila tu najiuliza nini kipo nyuma ya nguvu hii inayonishinda kujizuia?

Kilichonifanya nijione naingia katika hatari ni kwamba, juzi kushinda jana nilikwenda guest na msichana fulani nilikutana nae juu juu tu, tukafanya mapenzi na tulipomaliza wakati tunatoka kuna jitu la miraba minne lilikuwa likituangalia sana na yule msichana akashtuka sana.

Baadae nilipomuuliza akasema yule jamaa anafanya kazi na mume wake ni FFU kitengo cha doria.

Hakika nikaona hiki ni kifo cha wazi sasa na nimefikia pabaya, haya mambo sipangi ila imekuwa kama ulevi na siwezi kuacha.

Naombeni ushauri wa kunijenga wadau