Huenda Lady Jaydee akawa amepata mwanaume wa kumkabidhi moyo wake. Tangu aachane na mume wake, Gardiner G Habash, muimbaji huyo mkongwe hajawahi kuonekana na mwanaume aliyehisiwa kuwa ni mpenzi wake. Na sasa kwa picha alizoweka Instagram, uwezekano wa kuwa amerejea kupenda tena ukawa ni mkubwa.
Na tena kwa anachokiandika mwenyewe kwenye Instagram, Jide anamaanisha kuwa amefunga ndoa tayari! “Big shout out kwa Coastal air
Kwa kufanikisha safari yangu kwenda honeymoon #ZanzibarIsland,” ameandika Jide kwenye picha akiwa amesimama pembeni ya ndege waliyokodi na mwanaume huyo ambaye ni mgeni machoni pa wengi.
Kwenye picha nyingine hiyo juu, Jide ameandika: Thank you Serena Hotel for the amazing dinner 🙏 we really enjoyed #ZanzibarIsland.”
Pia rafiki yake wa siku nyingi, Monica Joseph ameweka picha za wawili hao na kuandika: My BFF is better than yours .. looking Good My People .. Love Lives here.”
Ni kweli Jide amefunga ndoa? Majibu yatapatikana punde!