Mmoja kati ya member wa ‘label’ ya WCB, Harmonize amethibitisha kuwa Rich Mavoko ni mmoja kati ya wasanii wa label hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Harmonize alisema label ya WCB ina wasanii watatu yeye mwenyewe , Raymond aliyekuwa Tip Top Connection pamoja na Rich Mavoko.
“Unajua mwanzo zilikuwa ni tetesi lakini naweza kusema ‘its official’ sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB,” alisema Harmonize
Aliongoza, “Kusema kuwa Rich Mavoko amenyoosha mikono kwa Diamond si vizuri kwani watu wanaweza kupata picha tofauti maana si unajua watu wanaweza kupokea jambo kwa maana na ikaleta picha mbaya wakati ni jambo la kawaida,”
23 Nov 2016
New
Sasa ni Rasmi..Rich Mavoko Asaini Katika Label ya ‘ WCB ‘ ya Diamond
mulo
Newer Article
Rich Mavoko Akana Kusign Mkataba wa Kuwa Chini ya Diamond..Atoa Ufafanuzi Hapa nini Kinaendelea Kwa Sasa
Older Article
Msanii Rich Movoko Amkana Mrembo Gigy Money 'Sikumbuki Hata Kukutana na Gigy Money Wala Kutoka Nae Kimapenzi Sinaga Upumbavu Huo'
Labels:
RICH MAVOKO,
WCB