Celline Dion Apiga Chini Dili Hili La Trump - MULO ENTERTAINER

Latest

31 Dec 2016

Celline Dion Apiga Chini Dili Hili La Trump


Siku si nyingi Rais mteule wa Marekani Donald Trump ataapishwa na kuanza kuitumikia ikulu ya taifa hilo la kwanza kwa ukubwa duniani. Kama ilivyo kawaida ya sherehe mbalimbali wasanii na watu maarufu hualikwa kwa ajili ya kutoa burudani,
tangu enzi za kampeni nchini marekani wasanii kibao wamekua wakimpinga Rais huyo mpya anaeshika nafasi ya Barrack Obama.

 Mtandao wa Us Weekly umeripoti kuwa muimbaji wa hitsong "My Heart Will Go On"   Celline Dion ameipiga chini ofa aliyopewa ya kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo zinazotarajiwa kufanyika January 20, 2017.