MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto wa kiume (Jayden), amesema mtoto huyo ameboresha mahaba niue kwa mpenzi wake, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza na Mikito Nusunusu, Chuchu alisema mtoto huyo amekuwa ni faraja kwao wote na mapenzi yameongezeka baina yake na mpenzi wake huyo kitu ambacho anamshukuru Mungu.
“Jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu, mahaba yamezidi asilimia ni jambo la kumshukuru sana aliye juu maana bila yeye kusingekuwa na kitu kabisa na ninamuomba atimize mambo mengine makubwa zaidi,” alisema Chuchu.