Spika Ndugai Awamulia Mawaziri wa Magufuli,Awachimba Mkwara wa Kufakuzisha Kazi,Soma Hapa Livee..!! - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Jan 2017

Spika Ndugai Awamulia Mawaziri wa Magufuli,Awachimba Mkwara wa Kufakuzisha Kazi,Soma Hapa Livee..!!


Wabunge na mawaziri wametii agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai lililowataka kuzingatia mahudhurio ya vikao vya kamati za Bunge, vinginevyo majina yao yangewasilishwa kwa mamlaka wanazowajibika ikiwamo kwa Rais  John Magufuli.


Katika mkutano wa nne wa Bunge mwaka jana, Spika Ndugai alisikitishwa na mahudhurio hafifu ya mawaziri na wabunge katika vikao vya kamati vilivyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 2 mjini Dodoma.

Amesema katika vikao hivyo vya kamati ilitengenezwa orodha ya wabunge na mawaziri watoro,  ambayo ataitunza hadi vikao vingine vya kamati.

Spika Ndugai aliwaonya kuwa  iwapo wataendelea na tabia ya utoro kwa vikao vya kamati vilivyofanyika kati ya Oktoba 17, 2016  angewashtaki kwa wapigakura, vyama vyao na mawaziri angewafikisha kwa Rais Magufuli.