Dear
Freeman Aikael Mbowe.
Salaamu na baada ya salamu,pole na mapambano ya kutufikisha "Canaan"
kupitia ukombozi wa pili wa Taifa hili... Najua fika ujasiri na uimara
wako wakati wote,sitishwi wala sijawahi kuwa na wasiwasi juu ya maamuzi
na kila hatua unayopiga kuelekea mbele.
Ndiyo maana nipokuwa upande mmoja na wewe sitishwi na upepo wa
kisulisuli,wala mvua za mabarafu,kwa kuwa najua ulivyosimama imara dhidi
ya dhoruba na vimbunga,vya kusi na tonadozi
Walipokupokonya vitega uchumi vyako ulicheka huku mikono umeweka
mifukoni,ukatuduwaza na kutuacha tukibubujikwa na machozi,walipokuja
kujachufua hotel yako na ukwepaji kodi,ulituambia umechoka kuonewa
huruma na kama hayupo tayari kukutana na haya tuachane na siasa za
upinzani Africa,wiki baadae tunaona wamekufuata mpaka kwenye bustani za
mchicha na nyanya,
Mimi na vijana wenzangu tulinyamaza kimya safari hii tukiogopa kufokewa
tena na wewe,na baadae tulikumbuka maneno yako ambayo ulikuwa
ukitusisitiza kuyakumbuka wakati wote. "Ni kweli wanaotutesa si wengi
kama sisi tunaoteswa,ila kuingiza nguvu wakati huu no kihatarisha maisha
ya wanyonge walioupande wetu,kwa nini tusisubirie watesi wetu wakiwa
mahala salama kwetu,kuepusha maafa"
Na kwamba jeshi zuri si lile linaloshinda vita tuh,bali ni lile
linaloshinda vita bila umwagaji damu na upotevu wa rasilimali zake
nyingi,ingawa siku zote vita huacha wahanga.
Dear Freeman Aikael Mbowe,nasubiria kwa hamu command yako ya
kusongambele,na nijaua si mimi tuh,nakuhakikishia vijana wenye utayari
ni zaidi ya mamillioni,waona jeshi la adui lipo nje ya geti letu je na
kuanza kuitikisa ngome yetu? Tuendelee kusubiria sauti yako kuu dhidi
yao?
Vijana wako tupo tayari kukulinda kwa gharama yoyote hata kama ni damu
na uhai wetu,ili makusudio ya ukombozi wa Taifa hili yafikie kama
ilivuokusudiwa.
Marehemu mawazo,alipata kusema "wanaotudhalilisha na kututesa sana wanatuharakisha sana,kufika tunapo elekea"
Tabia za vyombo vya dolla ni zilezile tuh,kizazi na kizazi avitoamka na kuwa upande wetu milele
Je tuendelee kusubiria lingine zaidi ya hili au wakati ni sasa,? Askari wako Mtiifu
BONIFACE JACOB
senior councillor UBUNGO
MJUMBE KAMATI KUU CHADEMA