Obama si mchoyo, amekuwa akizungumza katika vituo mbalimbali vya
televisheni na hata kwenye majukwaa kuwaeleza watu ni mambo gani
wanatakiwa kufanya ili wafanikiwe.
Haya hapa chini ni miongoni mwa mambo hayo ambayo kama ukiyafanya, hakika utafanikiwa;
JUA UTAFANIKIWA TU.
Kuhusu mafanikio, Obama anasema kama unataka kufanikiwa ni lazima ujue na kuamini kwamba utafanikiwa tu.
Wengine wamekuwa hawafanikiwi kwa kuwa hawajui kama watafanikiwa.
Alitolea mfano hai kwamba mwaka 1962, aliyekuwa Rais wa Marekani, John
Kennedy aliwaambia Wamarekani kwamba hawawezi kwenda mwezini kwa kuwa ni
mbali sana.
Lakini miaka saba baadaye Neil Armstrong akawa mwanadamu wa kwanza
kufika huko. Hivyo ndiyo ilivyo, wengine wameambiwa maneno mabaya kwamba
hawawezi kufika kwenye mafanikio kwa sababu tu wanaambiwa kwamba ni
vigumu, ndugu yangu, kuanzia leo jua kwamba utafanikiwa hata kama
kutakuwa na watu wengi wakizungumza maneno ya kukukatisha tamaa.
HUTAKIWI KURIDHIKA.
Obama anaendelea kusema kwamba ili ufanikiwe, hutakiwi kuridhika hata
kidogo. Wengine wamekuwa wakianguka au kutokufanikiwa kwa kuwa tu
waliridhika, waliingiza kiasi fulani cha fedha, wakajenga nyumba na
kununua magari wakaridhika.
Mafanikio si kununua gari tu, si kununua nyumba tu, bali ni kuwa na biashara nyingi ambazo zitakuingizia fedha kila siku.
UWE NA MALENGO.
Obama anasema kuwa, huwezi kufanikiwa bila kuwa na malengo. Ni lazima
unapoianza safari yako ujiwekee malengo kwani utakuwa ukifanya vitu
kuendana na malengo uliyojiwekea.
Kama hutaweka malengo, utakuwa unafanya vitu bila mpangilio wala
mwelekeo. Maisha ya mfanyabiashara ni lazima yawe na malengo ambayo
ndiyo ramani ya biashara yako na mafanikio yako kwa jumla.
HUWEZI KUFANYA PEKE YAKO.
Kwa mujibu wa Obama kama walivyo wengine wote wenye mafanikio, safari ya
mafanikio ni ndefu. Wengine wamekuwa wakihisi kwamba wanaweza kusimama
wakiwa
peke peke yao.
Ndugu zangu anachokisema Obama ni ukweli, huwezi kusimama peke yako
hasa kwenye masuala ya biashara na ndiyo maana mara kwa mara unasikia
kuna vikao vya wafanyabiashara. Utakapofanya kila kitu peke yako,
hutapata mawazo mapya kwa sababu utakuwa unaiamini akili yako pekee
katika kukufikisha sehemu f’lani.
Ili ufanikiwe, unatakiwa kuwashirikisha wafanyabiashara wenzako na
ikiwezekana, ukianzisha jambo, unaweza kuwaita na kuhitaji ushauri wao,
watakuwa msaada mkubwa kwako.
ACHA VISINGIZO.
Anasema kuwa wafanyabiashara wengine wamekuwa na kawaida ya kulalamika
hovyo. Wanaanzisha malengo yao, lakini mwisho wa siku wanakuja na
visingizio kwamba hawakufanikiwa kwa sababu fulani, hawakufanikiwa kwa
kuwa kulikuwa na watu waliowavuta nyuma kutoka kule walipokuwa
wakielekea.
Mfanyabiashara ukianza kutafuta visingizio, hutafika kwa sababu hakuna
mfanyabishara anayefanya biashara bila kupitia vikwazo mbalimbali
ambavyo usipokuwa makini ndivyo vitakavyokuwa visingizio. Kwamba,
hujafanikiwa kwa kuwa haukuwa na muda mrefu wa kazi au visingizio
vingine.
Unachokipata, kifanye tena kwa umakini mkubwa na kujitolea, achana na visingizio.
IFANYE BIASHARA YAKO IWE SERIOUS.
Obama anasema kwenye biashara kuna watu wanahisi kwamba wakiwa serious
mno ndiyo wanaweza kufanikiwa. Huwezi kufanikiwa kama utayafanya maisha
yako kuwa serious.
Matajiri wengi wanakuwa serious kwenye biashara na si maisha yao binafsi
ndiyo maana wanacheka na watu, wanataniana ili maisha yasonge lakini
kwenye biashara, huko ndipo unapotakiwa kuleta u-serious kupita kawaida,
kwani ukileta utani, utafeli.