Leo nimeona nilete elimu fupi juu ya makundi haya matatu ya watu waishio
hapa ulimwenguni, ambao ni MATAJIRI (The rich), WATU WA MAISHA YA KATI
(The middle class) na MASIKINI (The poor).
1.MATAJIRI
Nikianza na kundi hili, tafsiri halisi ya neno au kundi la watu hawa ni
tofauti sana na mtazamo wa waliowengi. matajiri ni wale watu ambao
humiliki Biashara kubwa au wamewekeza (invest) katika biashara kubwa na
ambapo hupata pesa ikiwa wapo au hawapo eneo husika. Pia kwa tafsiri
nyingine ni watu ambao pesa yao huwafanyia kazi au kuwaajiri watu
wengine wawafanyie kazi. mfano; Bill gates, Aliko dangote, Mo dewji n.k
(wawekezaji na wamiliki wa biashara kubwa)
2.WATU WA KIPATO CHA KATI
Hili ni kundi ambalo watu wengi hudhani kuwa ni matajiri lakini si kweli
na hii yote ni kutokana na mwenendo na hali ya maisha ya watu hawa.
Hapa nawazungumzia wale watu walio ajiriwa na kupokea mishahara minono,
wamiliki wa biashara ndogo, na wale wenye taaaluma(specialists or
talents) mbalimbali au kwa lugha nyepesi ni wale watu wanaotumia Muda,
Nguvu na Akili zao kupata kipato yaani kama ikitokea mtu huyu hayupo
eneo husika basi ndio unakuwa ukomo wa kupata kipato. mfano,
wanamichezo, waajiriwa.
3.MASIKINI
Hapa tunawakuta wale wote ambao hushindwa kutimiza mahitaji muhimu
katika maisha yao ikiwamo kula, kulala na hata mavazi yaani BASIC NEEDS
kwa lugha ya kiingereza. Na maisha ya kundi hili mara yingi yamekuwa ni
ya kukumbwa na simanzi, huzuni na kushindwa kupiga hatua kimaendeleo
kutokana na sababu kadha wa kadha.
Vilevile ningependenda kugusia swali fupi ''Kwanini Matajiri wanazidi
kuwa matajiri, Masikini wanazidi kuwa masikini na watu wa maisha ya kati
wanabaki hapohapo walipo siku zote?''
''why the rich get richer, the poor get poorer and the middle class are getting squezed out?''
Siri kubwa hapa si kitu gani watu hawa hufanya bali ni kitu/vitu gani watu hawa hununua.
Nikianza na MATAJIRI kundi hili mara zote wamekuwa ni watu wa kununua
vitegauchumi (assets) na ninaposema assets ama vitegauchumi simaanishi
nyumba ya kuishi, magari au vitu vingine vya thamani bali ni vile vyote
ambavyo ukinunua vinauwezo wa kukulipa (something that pays you money).
Mfano nyumba kwa ajili ya biashara (real estate), gari kwa ajili ya
biashara, Hisa (stocks), bond n.k
WATU WA MAISHA YA KATI (middle class) watu hawa hununua madeni yaani
(LIABILITIES) ninaposema madeni ni kwamba watu hawa hununua vitu ambavyo
hutoa pesa mifukoni mwao (somethings that cost money) mfano. gari la
kutembelea, nyumba ya thamani ya kuishi, tena vile vile wengine hata
hudiriki kuchukua mikopo bank ili wafanikishe hayo.
MASIKINI hawa siku zote hununua vitu ambavyo havina umuhimu sana maishani mwao.