Yumkini jaribio la mzee wa kiduku limeshtua sana Marekani ambapo sasa ni
rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The
Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana
tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo
la Florida nchini Marekani.
Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya
operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni
mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na
wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi
yote ya kimarekani.
Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana
popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe
barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni
Sea, Air and Land.
Ni Mara chache sana kutumika. Hawa ni tofauti na majeshi mengine kama US
Army Rangers, US Delta Force na mengine. Katika utawala wa Obama,
ametoa ruhusa MARA MOJA tu kwa US Navy Seal kutumika. Mara ya mwisho
kilitumika usiku wa manane kwa takribani dakika 45 tu kumuangamiza Osama
na ni askari mmoja tu alijeruhiwa kwa ajali ya helkopta zisizotoa sauti
ambayo ilikosewa ikagonga ukuta wakati makomandoo wakidrop kwenye
makazi ya Osama.
Na baada ya Operation Makomandoo hao waliilipua haraka helicopter yao
iliyopata hitilafu ili maadui wasigundue teknolojia iliyotumika
kutengenezea helicopter hiyo na baada ya kuilipua wakaondoka. Makomandoo
wa Navy Seal waliotumika katika Operation hiyo ni 11 tu na Marubani
Watatu ambao nao ni kutoka Navy Seal. Na ikumbukwe kuwa Operation hii
ilikuwa ikitazamwa live (mubashara) kutoka White House ambapo Obama
alikuwa akifuatilia (nilirusha tukio hili), kofia za makomandoo hawa
zilikuwa na kamera mbele ambazo zilitumika kurekodi kila kitu
kinachoonekana mbele na kurusha kwenye satelaiti had White House.
Mkakati huu ulisimamiwa na Mwanamke hatari zaidi anayejulikana kama
Alfreda Frances Bikosky ambaye ni Afisa mwandamizi wa CIA na jasusi
aliyebobea na pia ni komandoo lakini si memba wa Navy Seal. Bibi Alfreda
anajulikana zaidi katika jeshi la Marekani kama MALKIA WA MATESO.
Serikali ya Marekani inajitahidi kudhibiti mitandao ya kijamii na google
isisambaze picha za mama huyu hatari.
Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya makomandoo wengine wa
majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem husika, ramani ya
ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa ruhusa ya NAVY
SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za Navy Seal
ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea),
Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue
(kama walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa
Kimarekani waliotekwa Iran) na Foreign Internal Defence.
Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985 ambao ni hatari mno na
wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye mazoezi makali
ya special operations na trainings ngumu muda wote huko Virginia,
Marekani. Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA kufanya
kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa. Makamu wa Rais wa Marekani Bwana
Pence yuko Korea Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY
SEAL waliojichimbia katika Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya
Korea..