Mwanamuziki wa injili, Upendo Nkone amesema yuko tayari kutumikia nafasi
ya ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo Rais
Magufuli atamteua.
Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema, anaamini
ametumwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kupitia uimbaji, lakini pia yuko
tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge, na kuweka wazi kuwa
si kwa ubunge wa kugombea jimboni.
"Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi,
lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti
maalum, kwakweli napokea.... Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge,
basi unikumbuke baba" Amesema Upendo
Amesema aliwahi kushauriwa kugombea ubunge katika jimbo fulani lakini hakuwa tayari kwa kuwa hapendi kugombea.
Akieleza sababu kuu ya kutopenda ubunge wa kugombea, amesema masharti ya
kugombea ni lazima uwe kwenye vyama vya siasa jambo ambalo halipendi.
Jambo lingine amesema mchakato wa kupata ubunge wa kugombea ni mgumu una
mambo mengi ikiwa ni pamoja na gharama, jambo ambalo haliwezi na hivyo
kusisitiza kuwa Rais Magufuli anapaswa kumkumbuka katika nafasi zake za
kutea