Najua wengi wana tatizo la makwapa kuwa meusi tii hadi wanaogopa kuvaaa
vijiguo wazi maana lol. Sasa hapa nakupa some tips zakuondoa huo weusi
katika makwapa. Hapa ni njia 3 za kukusaidia; tumia ile iliyo karibu
zaidi na wewe.
Baking Soda
Changanya baking soda na maji.
Weka au paka hapo kwenye kwapa jeusi
Acha kwa dakika 10 – 15
Osha na maji ya vugu vugu
Uwe ukifanya hivyo mara kadhaa katika wiki utaona tatizo lako linakwisha
Apple Cider Vinegar
Pakaa hiyo apple cider vineger
Baada ya dakika 5 futa na kitambaa cha cotton – usioshe na maji
Viazi ulaya
Kiponde ponde
Kisha pakaa uji wake katika kwapa
Acha kwa dakika 30 kisha osha vizuri
Haya nimekupa hizo tiba tatu tofauti kuondokana na kwapa jeusi please.