Kuna wakati unaweza kujikuta hauko vizuri kila siku na ukashindwa kujua nini tatizo.
Sasa leo napenda tujuzane hizi dalili ambazo ikiwa utaziona basi huenda ukawa na matatizo kiafya:-
1. Kupungua uzito ghafla.
Kuna baadhi ya watu huweza kujikuta ghafla tu wamepoteza kilo kadhaa
bila kuwepo na sababu za msingi, hivyo wataalam wa afya wanashauri
inapotokea hali hiyo ni vyema kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini sababu
za msingi za hali hiyo kutokea.
2. Mabadiliko ya ngozi.
Ngozi ni alama tosha ambayo huashiria uwepo wa afya bora kwa binadamu
hivyo basi ikiwa utaona ngozi yako imeanza kupoteza uhalisia wake basi
ujue huenda tayari kunatatizo la kiafya linakunyemelea hivyo unaweza
kuwaona wataalam kwa ushauri zaidi.
3. Mabadiliko ya haja ndogo
Unapoona kuanza mabadiliko ya haja ndogo au haja kubwa basi huenda nayo
ikawa dalili ya tatizo, hivyo ni vyema kuwa mchunguzaji wa haja zako ili
kung'amua baadhi ya matatizo ya kiafya kwa haraka na kuyatafutia
ufumbuzi kwa wataalam.
4. Matatizo ya kukosa usingizi.
Hii nayo huweza kuwa ni kiashiria cha tatizo mwilini mwako hivyo
unapoona mabadiliko yanahusu usingizi pia unaweza kujichunguza vizuri na
unapoona huelewi basi waone wataalam kwa ufafanuzi zaidi.
5. Midomo kukauka.
Unapoona midomo inakauka au kupasuka nayo huweza kuwa dalili mbaya
kiafya hivyo unaweza kufanya maamuzi ya kwenda kufanya uchunguzi wa
kiafya ili kujua tatizo zaidi.
6. Mabadiliko ya joto la mwili
Iwapo mwili unakuwa na joto mara kwa mara nayo huweza kuwa ni moja ya
kiashiria cha tatizo kiafya, hivyo ni vyema kuwaona wataalam kwa ajili
ya uchunguzi zaidi wa kiafya.
7. Unapokosa hamu ya kula kabisa
Nayo ni moja ya dalili kuwa mwili wako unashida hivyo ni muhimu kufika kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
8. Uchovu wa mwili
Mwili unapojihisi umekuwa mzito nayo huwa dalili ya tatizo ndani ya
mwili wako nayo si vizuri kuipuuza na badala yake ni vyema kufanya
uchunguzi zaidi.