Mugabe Aishangaza Dunia...Atangaza Msamaha Kwa Raia wa Zimbabwe Waliowaua Wazungu - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Aug 2017

Mugabe Aishangaza Dunia...Atangaza Msamaha Kwa Raia wa Zimbabwe Waliowaua Wazungu

Mugabe Aishangaza Dunia...Atangaza Msamaha Kwa Raia wa Zimbabwe Waliowaua Wazungu
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametangaza kuwa raia wote wa nchi hiyo waliokuwa wakituhumiwa kuwaua wazungu waliokuwa wakifanya biashara katika mashamba tangu kuanza kwa programu ya mabadiliko ya ardhi mwaka 2000, hawatoshtakiwa.

Akizungumza mbele ya umati wa watu katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa, Mugabe alisema wazungu hao waliuawa kwa sababu walipinga agizo lililokuwa limewekwa na serikali.

“Kuna waliouawa wakati walipoleta ubishi. Hatutokaa tuwashtaki wale wote walioawaua. Nauliza; Kwanini tuwakamate?” aliuliza Rais Mugabe wakati akihutubia wananchi.

Takribani wazungu 12 waliokuwa wakijihusisha na kilimo katika mashamba ya biashara waliuawa na wanaodaiwa kwamba ni wanaharakati wa Chama cha ZANU-PF na wapiganaji vita wastaafu wakati wakugombea mashamba, tukio lililotupiwa lawama na mataifa mbalimbali.

Tukio hilo lilisababisha pia mataifa ya magharibi kumuwekea vizuizi Rais Mugabe asiweze kusafiri kwenda katika nchi hizo wakimtuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na umiliki mali.

Mugabe amewaambia wajumbe wa mkutano wa mwaka wa ZANU-PF kwamba, hakuna uamuzi wa mahakama utakaobatilisha namna walivyoamua kupata ardhi yao. Alisema kuwa, hata hivyo, ardhi ni yao kwa haki ya kuzaliwa, kama raia ni haki yao, na ni yao kwa kuipigania.

Rais Mugabe amewataka raia wa taifa hilo ambao wamepata ardhi kutokodisha kwa wakulima wakizungu.

“Wakati mwingine wakulima wa kizungu wanarudi kuja kukusanya matrekta yao au kutaka kushirikiana na wakulima wapya. Wakulima wapya wanalaghaiwa bila ya wao kujua.”

Mugabe alisema kwamba taifa hilo halikuwahi kutaka kuwafukuza raia wa kigeni (wazungu) nchini humo na kwamba walioondoka walifanya hivyo kwa maamuzi yao wenyewe.

Alieleza kwamba, takribani watu 100,000 ambao ni wazungu wapo nchini humo kati ya 250,000 waliokuwepo wakati nchi hiyo inapata uhuru.