Ni siku mbili zimepita tangu Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu aliposhambuliwa kwa risasi nyumbani kwake Dodoma ambapo leo September 9, 2017 Polisi imekutana na Waandishi wa habari kueleza kinachoendelea.
Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi na Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto ndio ameongea na kusema kuna Watu 30 wamekamatwa kwa makosa mbalimbali yaliyotokea Dodoma.
Amesema magari 8 pia yamekamatwa aina ya Nissan na Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kubaini ni kina nani wamefanya shambulizi hilo kwa Tundu Lissu ambapo Jeshi la Polisi bado linaendelea kutoa wito kwa Wananchi wenye taarifa za tukio hilo waendelee kuzifikisha Polisi.
Lakini Jeshi hilo limeagiza Dereva wa Tundu Lissu kujisalimisha Polisi haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uchunguzi wa awali kuhusiana na tukio ambapo kamanda Muroto amesema…>>>”Polisi inamtaka dereva wa Tundu lissu ajitokeze na afike Polisi Dodoma bila kukosa au makao makuu ya upelelezi Dar es salaam ili aweze kutoa maelezo” –RPC Muroto
“Kutoweka kwake na kujificha ni kosa la jinai na kama kuna mtu au watu wanamficha wanatenda kosa la jinai, wamfikishe Polisi bila kukosa kwa kuwa ni shahidi muhimu katika upelelezi” –RPC Muroto
10 Sept 2017
New