Zitto Ataka Uchunguzi wa Kujitegemea Kutoka Nje Sakata la Lissu...Adai Vyombo vya Ndani sio vya Kuamini - MULO ENTERTAINER

Latest

9 Sept 2017

Zitto Ataka Uchunguzi wa Kujitegemea Kutoka Nje Sakata la Lissu...Adai Vyombo vya Ndani sio vya Kuamini

Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo Zitto Ruyagwa Kabwe ameungana na kauli iliyotolewa leo na Baraza la Vijana la CHADEMA kuitaka serikali kutia uzito uchunguzi wa jaribio la kuuliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusu vyombo vya kimataifa


Kwenye ukurasa wake wa twitter Zitto Kabwe amendika ujumbe akivitaka vyombo vingine vya kimataifa kufanya uchunguzi juu ya shambulio la Tundu Lissu, kwani haviamini vyombo vya ndani.

"Natafuta uchunguzi wa kujitegemea kimataifa juu ya jaribio la mauaji dhidi ya Mbunge Tundu Lissu, vyombo vya ndani sio vya kuviamini", aliandika Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe aliendelea kwa kuandika kwamba watu waliofanya tukio hilo wana lengo la kuwafunga midomo wanapopaza sauti zao kupinga uonevu, hivyo hawatakiwi kukaa kimya kwani watakuwa wamewapa ushindi.

Leo asubuhi Baraza la Vijana CHADEMA limefanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia tukio la kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu, na kuitaka serikali itie uzito jambo hilo kwa kuunda tume huru maalum ya kuchuguza, pamoja na vyombo vya kimataifa.