Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka wazi msimamo wake huo wa kutoyumbishwa na watu hao ambao wameanza kusambaza taarifa mbalimbali kuhusu Zitto Kabwe na kusema hizo ni ajenda wanazofanya kutaka kumtoa kwenye mstari wa sakata kuhusu wahusika halisi ambao wamefanya shambulio la risasi kwa mbunge Lissu
"Hizi ni propaganda za dola ili kuhamisha mjadala kuhusu wahusika halisi wa shambulio la risasi dhidi ya Mbunge Tundu Lissu. Sitawapa muda" alisisitiza Zitto Kabwe