LICHA ya hivi karibuni kujinadi kuwa ametupia wigi la bei mbaya alilodai kulinunua kwa shilingi milioni sita, msanii wa Bongo Fleva anayefanya poa na ngoma yake ya Nampa Papa, Gift Stanford ‘Gigy Money’ anadaiwa kuishi kwenye nyumba ambayo haina hadhi ya hilo wigi hivyo kuibua miguno.
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilifika kwenye nyumba hiyo anayoishi Gigy maeneo ya Sinza-Kwaremi jijini Dar na kushuhudia inavyoonekana kwa nje kuwa haina hadhi, lakini kwa ndani ni bonge la nyumba.
Chanzo makini kilieleza kwamba, mwanadada huyo anaishi maeneo hayo kwenye nyumba hiyo yenye muonekano kama banda ambapo siyo hadhi yake, hali inayowashangaza wengi kutokana na umachachari wake hivyo kujiuliza inakuwaje ashindwe kuishi kwenye mjengo wenye hadhi yake.
“Yaani Gigy anaishi kwenye banda maana muonekano wa nyumba anayoishi kwa kweli unashangaza na hapa mtaani watu wamekuwa wakimsema sana na kumshangaa kwamba inakuwaje aishi hivyo wakati ni staa mkubwa ambaye anafanya shoo na kupata fedha?” kilihoji chanzo hicho.
Akizungumzia ishu hiyo katika mahojiano maalum na gazeti hili, Gigy alisema hawezi kuwakataza watu kuongea kwa sababu nyumba hiyo alijilipia kodi mwenyewe kwa mapenzi yake na wala hakulazimishwa na mtu.
“Ninawashangaa sana watu wanavyochonga wakati kwa ndani nyumba hii ni nzuri kabisa. Nadhani ninyi wenyewe mnajionea hii nyumba ilivyo kubwa.
“Kwanza hapa nimepanga nyumba nzima, ina sebule, jiko, chumba, choo, sehemu ya kuweka nguo na bado ina uwanja mkubwa wa magari hata matano.
“Sasa kwa nini nisiridhike kukaa hapa? Wasanii wengi wamepanga chumba kimoja, waliopanga nyumba nzima kama mimi ni wachache mno. Kwa nini nikapange jumba la kifahari wakati sina hata kibanda? Si ni bora hiyo pesa nijenge nyumba yangu!” aliwaka Gigy.
Hata hivyo, katika kile kinachoonesha Gigy anakerwa na maneno hayo, aliwataka mapaparazi wetu wakague nyumba nzima kujiridhisha anachoongea ambapo walibaini muonekano wa nje wa nyumba hiyo ndiyo hauvutii, lakini kwa ndani hakuna tofauti ya makazi anayoishi na umaarufu alionao.