Mtalaka wa Sugu Azuiwa Kuingia Ofisi za RITA Kisa Maadili... - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Jan 2018

Mtalaka wa Sugu Azuiwa Kuingia Ofisi za RITA Kisa Maadili...


Mtalaka wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi "Sugu", Faiza Ally alijikuta akizuiwa kuingia katika ofisi za RITA jijini Dar es Salaam kutokana na kuvaa mavazi yasiyo na staha.

Askari waliokuwepo ofisi za RITA walimtaka Faiza Ally akabadili vazi na kuvaa linalostahili kuvaliwa katika ofisi ya umma. Baada ya mvutano, alijitokeza msamaria aliyemuazima mtandio ambao alivaa na ndipo aliporuhusiwa kuingia ofisini ili kutimiziwa shida iliyompeleka.