Picha za Utupu, Basata Wamkimbiza Bongo Pretty Kind. - MULO ENTERTAINER

Latest

12 Jan 2018

Picha za Utupu, Basata Wamkimbiza Bongo Pretty Kind.

Picha za Utubu, Basata Wamkimbiza Bongo Pretty Kind
MSANII wa filamu Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ amepanga kutimkia nchini India alipokuwa anaishi siku chache zilizopita kwa bwana’ke, baada ya kupigwa kufuli na Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kutokana na kuweka picha zisizo na maadili mtandaoni (nusu utupu).

Kwa mujibu wa chanzo chetu, baada ya mwanadada huyo kupewa agizo hilo na serikali alipagawa na kuona haoni faida ya kuendelea kuwepo Bongo kwa kipindi hicho kwa kuhofia kuchekwa na watu na kuona bora arudi India kwa mwandani wake aliyekuwa akiishi naye miaka ya nyuma.



Alipotafutwa na paparazi wetu, Pretty alifunguka: “Ni kweli najiandaa ‘soon’ naenda India, maana masharti niliyopewa ni magumu mno kuambiwa hata picha nisiweke mtandaoni imeniuma sana, ili nitii vizuri hili agizo nimeona bora nisiwepo hapa nchini, adhabu ikiisha nitarudi.”