RC Makonda Aingilia Kati Mgogoro wa Nyumba ya Mjane Ataka Isipigwe Mnada - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Jan 2018

RC Makonda Aingilia Kati Mgogoro wa Nyumba ya Mjane Ataka Isipigwe Mnada

RC Makonda Aingilia Kati Mgogoro wa Nyumba ya Mjane Ataka Isipigwe Mnada

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza mjane Bernadetha Ryewendera mkazi wa Tegeta Mtaa wa Upendo asibughudhiwe, aachwe aendelee kuishi kwenye nyumba yake ambayo ilipigwa mnada kinyume cha sheria bila yeye kuwa na taarifa rasmi.


Hayo yamejiri leo Jumatatu, Januari 15, kufuatia video ya mama huyo kusambaa mitandaoni ikimuonyesha akilalamikia baada ya nyumba yake kupigwa mnada, ambapo Makonda aliagiza mama huyo atafutwe na afike ofisini kwake leo saa tatu asubuhi jambo ambalo mama huyo ameliekeleza.

Mjane huyo ambaye anadai nyumba yake ilipigwa mnada January 12 mwaka huu kwa dakika tano bila yeye kupewa taarifa yoyote, amefika ofisini kwa Makonda leo ambapo baada ya kupitia nyaraka zake, RC Makonda ameagiza kusimamisha mnada wa nyumba hiyo aliouita ni batili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Makonda amesema kuwa katika uchunguzi wa awali uliofanywa na wanasheria umeonyesha kuna utapeli mkubwa uliofanywa ambapo nyaraka zimegushiwa sahihi ya Bi Zainabu Kaswaka ambaye ni mmiliki wa eneo alilouziwa Bi Rweyendera. Imeelezwa pia kuwa nyumba iliyopigwa mnada ilikuwa na zuio mahakamani tangu mwaka jana.

Aidha Makonda ameagiza watuhumiwa wa utapeli huo kukamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria mara moja.