NIDA Yaanza Zoezi la Kuweka Pingamizi kwa Waliojiandikisha Vitambulisho vya Taifa - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Jan 2018

NIDA Yaanza Zoezi la Kuweka Pingamizi kwa Waliojiandikisha Vitambulisho vya Taifa

NIDA Yaanza Zoezi la Kuweka Pingamizi kwa Waliojiandikisha Vitambulisho vya Taifa

January 15, 2018 zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea kufanyika Mkoani wa Songwe ambapo wananchi wameonyesha mwamko wa kujitokeza kukamilisha jukumu lao la msingi la kujisajili ili kupata Vitambulisho ukiachia mbali mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani humo.


Afisa usajili wa Songwe Coletha Peter amesema kwasasa wanaendelea na Usajili katika Wilaya ya Mbozi na wako kwenye awamu ya 5 wanayotegemea kumaliza January 20, 2018.

Amesema baada ya kukamilika kwa awamu ya 5 wataingia katika awamu ya 6 itakayohusisha kata ya Nambizo, Magamba, Nanyala na Ruanda na kuwasititiza Wananchi wa kata zilizo katika awamu ya 6 kujiandaa kwa zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa Viambatanisho vya msingi vinavyohitajika katika zoezi la Usajili na Utambuzi.

Katika mkoa wa Songwe Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza zoezi la mapingamizi ambapo wananchi wanapata fursa ya kuhakiki taarifa zao pamoja na kuweka mapingamizi kwa mtu yoyote wanayehisi si raia au si Mkazi wa eneo husika na amefanya usajili wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, ambapo Coletha amewasihi Wananchi wa kata Ichenjezya, Vwawa na Mlowo ambazo ndo zimeanza zoezi hilo, kuwa wazalendo katika kufanikisha zoezi hilo.