Watu 12 Wafariki Kwenye Ajali ya Gari Mkoani Kagera - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Jan 2018

Watu 12 Wafariki Kwenye Ajali ya Gari Mkoani Kagera

Watu 12 Wafariki Kwenye Ajali ya Gari Mkoani Kagera

AJALI mbaya ya gari dogo aina ya Nissan Caravan (Hiace) lenye namba za usajili T 542 DKE ambalo limegonga magari makubwa mawili ya mizigo imesababisha vifo vya watu 11 na wengine watano kujeruhiwa katika eneo la Nyangozi kata ya Nyantakara wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera jana Jumapili, Jan. 14, 2017.


Kamanda waPolisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambap ameeleza kuwa gari hilo dogo la abiria lilikuwa linatokea Kakonko mkoani Kigoma kuelekea Kahama huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva ambaye aligonga magari mawili ya mizigo yenye namba za usajili T694 COX lililokuwa likivuta tela namba T 103 DKJ mali ya kampuni ya Mruruma Enterprises ya Dar es Salaam.

Ollomi amesema kuwa watu 9 wamefariki papo hapo eneo la ajali, mmoja alifariki njiani akiwahishwa hospitali na mwingine amepoteza maisha leo asubuhi. Majeruhi watano wanaendelea kupata matibabu katika hospitali teule ya Wilaya ya Biharamulo.

Gari hilo dogo lilikuwa na abiria wapatao 17 ambapo 11 wamefariki akiwemo dereva wake na watano wamejeruhiwa huku mmpoja akitoka salama.