Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Mvumo wa Radi’ ameiambia ITV kuwa kuna uwekano wa albamu kutoka mwaka huu na tayari maandalizi yameshafanyika.
“Albamu naweza nikaachia mwaka huu nipo katika kumalizia japokuwa tayari nipo na nyimbo ila nataka kila kitu kitoke kikiwa perfect,” amesema Alikiba.
Ameongeza kuwa albamu hiyo itauzwa kwa njia ya online na kawaida, yaani hard copy.
Utakumbuka kuwa wasanii wa Bongo Flava waliotoa albamu hivi karibuni ni pamoja na Vanessa Mdee, Diamond, Wakazi na Chin Bees.
26 May 2018
New